MigogoroMamlaka ya Palestina
Hamas: Vitisho vya Trump vyaathiri makubaliano yao na Israel
7 Machi 2025Matangazo
Kiongozi huyo wa Marekani amewataka Hamas kuwaachilia huru mateka wote wa Israel la sivyo watu wa Gaza wataangamizwa.
Onyo hilo la Trump, limetolewa saa chache baada ya serikali yake kuweka wazi kwamba imefanya mazungumzo na kundi hilo la Hamas ambalo imeliita ni kundi la kigaidi,
Mazungumzo yao yalijikita kwenye suala la mateka wa Marekani wanaoshikiliwa Gaza. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu pia imethibitisha kwamba ilishauriwa na Marekani na kutowa mtazamo wake.