Hamas na Israel wabadilishana mateka na wafungwa
22 Februari 2025Matangazo
Awamu hiyo ya pili itatakiwa kuendeleza hatua za kubadilishana mateka na wafungwa na kusitisha kabisa vita huku vikosi vya Israel vikijiondoa kabisa katika Ukanda huo.
Hamas yawaachilia mateka wawili
Leo Jumamosi, Hamas imewaachia huru mateka wawili wa Israel waliofahamika kama Tal Shoham na Averu Mengistuna na kuwakabidhi kwa wafanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu huko Rafah.
Mateka wengine wanne, Omer Shem-Tov, Eliya Cohen, Omer Wenkert, na Hisham al-Sayed, wanatazamiwa kuachiliwa baadaye leo huko Nuseirat katikati mwa Gaza. Israel itatakiwa pia kuwaachilia mamia ya wafungwa wa Kipalestina.