Hamas kumuachia huru mateka wa Israel
12 Mei 2025Kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza limesema litamuachia huru leo, mateka wa mwisho ambaye yuko hai, raia wa Marekani na Israel anayeshikiliwa huko Gaza.
Kundi hilo lilitowa taarifa hiyo jana Jumapili, bila ya kutowa ufafanuzi zaidi kuhusu hatua hiyo, na kusisitiza kwamba litamuachia huru, Edan Alexander kama ishara ya nia njema kwa utawala wa rais Donald Trump.Soma pia:Mpango wa Marekani juu ya misaada ya kiutu Gaza wapingwa
Israel imesema maandalizi yameshafanywa ya kumpokea mateka huyo mchana wa leo Jumatatu, kwa mujibu wa vyombo vya habari.Soma pia: Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani atoa wito wa amani
Awali ofisi ya Waziri mkuu Benjamin Netanyahu ilisema kwamba mpango huo wa kuachiliwa raia wake Alexander unatarajiwa, ingawa haikuweka wazi wakati gani tukio hilo litafanyika.