Hamas itatoa majina ya mateka wanne watakaoachiwa karibuni
24 Januari 2025Naim, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas iliyoko Doha, amesema wanawake hao wataachiliwa kwa kubadilishana kwa kundi la wafungwa wa Kipalestina, na mara baada ya mabadilishano hayo, Wapalestina waliofurushwa na vita kusini mwa Gaza wataweza kuanza kurejea kaskazini mwa eneo hilo.
Huku haya yakijiri familia za mateka wa Israel zilimtaka Rais wa Marekani Donald Trump kuendeleza juhudi za kidiplomasia hadi mateka wote wanaoshikiliwa huko Gaza waachiliwe.
Gavana: Watu wanakimbia operesheni ya Israel mji wa Jenin
Ayelet Samerano, mama yake mateka mmoja anayeshikiwa Gaza asema:
“Mpendwa Rais Donald Trump. Kwanza kabisa, tunataka kusema asante kwa nyakati za furaha tulizohisi wiki hii. Lakini tunataka kukuambia, bado kuna mateka 94. Tunawahitaji wote nyumbani. Tafadhali usisitishe. Tafadhali endelea, kusisitiza na ufanye kila kitu. kwamba mateka wote 94 warudi nyumbani mara moja."
Aidha wameitaka serikali ya Israel kuendelea na hatua ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano hadi mateka wote watakapoachiliwa.