Hamas yaangalia upya mapedekezo ya amani ya Gaza
2 Julai 2025Awali Kundi hilo la wanamgambo lilisema lipo tayari kukubali usitishaji mapigano na Israel, lakini halikuwa tayari kuukubali mpango ulioungwa mkono na Marekani uliotangazwa na Rais Donald Trump hivi karibuni, likisema linashikilia msimamo wake wa muda mrefu, kuwa makubaliano yoyote ni lazima yajumuishe kusitisha kikamilifu vita katika Ukanda huo wa Gaza.
Jeshi la Israel latangaza kutanua operesheni za kijeshi Gaza kabla ya ziara ya Netanyahu, Washington
Rais Trump, alisema Israel imekubali kusitisha vita kwa siku 60 mjini Gaza, na kulihimiza kundi la Hamas kuridhia mpango huo kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Rais huyo wa Marekani amesema siku hizo 60 zitatumika kuendeleza juhudi za kumaliza kabisa vita, jambo ambalo Israel inasema haitowezekana hadi ilisambaratishe na kulishinda kundi la Hamas.