Hamas imeukataa mpango wa Israel wa kuhamisha wakazi wa Gaza
17 Agosti 2025Matangazo
Aida kundi hilo limekiita kitendo cha Israel wa kuweka mahema na vifaa vingine vya makazi katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza ni "udanganyifu wa wazi".Wakati hayo yakiarifiwa, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliwashutumu waandamanaji kote nchini Israel, wanaodai vita ya Gaza ikome, akisema wanaupa nguvu msimamo wa Hamas katika meza ya mazungumzo.Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya waziri mkuu huyo inasema "wanaotaka vita ikome leo bila kushindwa kwa Hamas si tu wanatia nguvu msimamo wa Hamas na kuchelewesha kuachiliwa kwa mateka wetu, bali pia wanatoa hakikisho la kuwa matukio ya kutisha ya Oktoba 7 kutokea tena."