MigogoroMashariki ya Kati
Hamas imekabidhi miili ya mateka wanne wa Israel
20 Februari 2025Matangazo
Miili ya mama aliyefahamika kwa jina Shiri Bibas na wanawe, wawili Ariel na Kfir, na mateka mwingine Oded Lifshitz aliyekuwa na umri wa miaka 83 wakati akitekwa nyara, imeachiliwa kutoka Ukanda wa Gaza katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la zamani la makaburi ya mji wa Khan Yunis.
Soma pia:Hamas yakabidhi miili 4 ya mateka wa Israel
Kundi la Hamas limesema wote waliuwawa katika shambulio lililofanywa na Israel mwanzoni mwa vita vya Gaza. Jana waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema, taifa zima liko kwenye masikitiko wakati likisubiri kurejeshwa kwa miili ya raia hao.