Mapigano mashariki mwa Kongo yanazidi kuongezeka, huku waasi wa M23 wakiendelea kuutishia mji wa Goma na serikali ya Kongo ikiwarejesha wanadiplomasia wake kutoka Rwanda, na kushtumu Kigali kuwa na dhamira ya kuiteka Goma kwa kujificha nyuma ya M23. Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo Jumapili katika kikao cha dharura kujadili hali inayozidi kuwa tete Kongo.