Hali ya Papa Francis inaendelea kuimarika
16 Februari 2025Matangazo
Papa Francis amelazwa katika hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Rome na anapokea matibabu kutokana na kupata maambukizi kwenye njia ya upumuaji.
Taarifa ya makao makuu ya kanisa Katoliki, Vatican imesema Papa Francis hatoweza kujitokeza hadharani hii leo Jumapili kuongoza ibada ya wiki kwa sababu madaktari wamemtaka kiongozi huyo wa Kanisa katoliki apumzike.
Papa Francis kuondoka hospitali Jumamosi baada ya kupata nafuu
Vatican imesema Papa Francis ataendelea kuwa hospitalini kwa muda kwa ajili ya kupokea matibabu.