Saba Saba yaadhimishwa kwa maandamano Kenya
7 Julai 2025Matangazo
Saba Saba inadhimishwa kila Tarehe 7 Julai kuwakumbuka waliopigania demokrasia na mfumo wa vyama vingi nchini Kenya mwaka 1990, baada ya kupitia miaka mingi ya utawala wa kiimla kutoka kwa rais wa wakati huo Daniel Arap Moi.
Mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika wakati vijana wa kenya maarufu kama Gen Z waliokasirishwa na hali ya uchumi kudorora, rushwa na vitendo vya mara kwa mara vya ukatili wa polisi dhidi yao, wakiandamana kutaka mageuzi serikalini.
16 wauawa kwenye maandamano ya GenZ nchini Kenya
Hata hivyo waandamanaji wameishutumu serikali kuwalipa magenge ya wahalifu kuvuruga maandamano yao waliyoyaita ya amani. Serikali nayo imesema maandamano hayo yamepangwa na baadhi ya wanasiasa kwa nia ya kuipindua.