MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Hali bado ni tete nchini Kongo, Guterres aomba amani
7 Februari 2025Matangazo
Kundi la waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waliendelea kusonga mbele jana Alhamisi katika eneo la mashariki mwa Kongo na walionekana wakijiandaa kuuteka mji muhimu wa kimkakati, wakati katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitaka pawepo amani.
Akizungumza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Guterres amesema ni wakati wa kuufikisha mwisho mgogoro huo.
Pia alisema tuko katika wakati muhimu na ni wakati muafaka wa kuungana pamoja kwa ajili ya amani. Wakati haya yakiarifiwa, rais wa Kongo, Felix Tshisekedi atashiriki mkutano wa pamoja wa kilele wa viongozi wa mashariki na kusini mwa Afrika unaoanza leo hadi kesho jijini Dar es Salaam, Tanzania kujadili mgogoro wa mashariki mwa Kongo.