Guterres aahidi kuunga mkono ujenzi mpya wa Ukraine
1 Julai 2025Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterresametoa ahadi ya msaada kwa Ukraine, ambayo inashambuliwa na Urusi kwa zaidi ya watatu, lakini ni kwa kile alichosema kwa juhudi zinazowezekana za ujenzi.
Wakati wa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal, katika kipindi cha Mkutano wa nne wa Umoja wa Mataifa juu ya Ufadhili wa Maendeleo wa huko Seville, kusini mwa Uhispania, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitangaza dhamira ya kuunga mkono juhudi za serikali ya Ukraine kushughulikia mahitaji ya kibinadamu, ujenzi na uokoaji.
Soma zaidi:Papa Leo ataka Sheria za kimataifa ziheshimiwe Mashariki ya Kati
Guterrespia alisisitiza umuhimu wa kufikiwa ukamilifu, kusitishwa mapigano mara moja na bila masharti nchini Ukraine. Akisema hiyo itakuwa hatua ya mwanzo kuelekea amani ya haki, kwa upana wake na endelevu, ambayo inaheshimu kikamilifu Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na Maazimio ya Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa.