Guterres: Ni uhalifu kwa Marekani na Ulaya kusitisha misaada
14 Machi 2025Matangazo
Guterres amesema hayo wakati wa ziara ya siku nne nchini Bangladesh ambapo anatathmini masaibu ya zaidi ya wakimbizi milioni 1 wa Rohingya ambao mustakabali wao haujulikani kutokana na uwezekano wa kupunguzwa kwa misaada hiyo hivi karibuni.
Guterres ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utafanya linalowezekana kupanga ufadhili wa kutosha kwa wakimbizi hao wa Rohingya baada ya tangazo hilo la hivi karibuni zaidi la kupunguzwa kwa misaada.
Katika mkutano na kaimu kiongozi wa Bangladesh, ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Muhammad Yunus katika mji mkuu Dhaka, Guterres alielezea wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa mataifa ya Magharibi kuongeza bajeti ya ulinzi huku yakibana misaada ya kibinadamu kote ulimwenguni.