Guterres: Haki za binadamu zimebinywa na watawala wa kiimla
24 Februari 2025Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema haki za binaadamu zimedhoofishwa mno kote ulimwengunina madikteta na watu wanaopenda vita, hali inayozidisha migawanyiko na ghadhabu.
Kwenye hotuba yake mbele ya Baraza la Haki za Binaadamu la umoja huo, Guterres amesema haki za binaadamu zimeminywa na madikteta wanaokandamiza upinzani kutokana na hofu ya kile wanachoweza kufanyiwa na watu.
Amezungumzia kuanzia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine huku akitoa wito wa makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano huko Gaza. Aidha ameomba kuheshimiwa kwa uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amependekeza mawazo mapya kwenye Baraza la Usalama ili kuleta utulivu na usalama kwa watu wa Haiti, ambako Umoja huo umepeleka ujumbe wa amani.