Guterres azitaka nchi wanachama wa UM kulipa michango
13 Mei 2025Amesema hilo lisaidia shughuli za kulinda amani kote duniani hususani nyakati hizo ambazo "ulimwengu unashuhudia idadi kubwa ya mizozo".
Guterres ameuambia mkutano wa mawaziri unaofanyika nchini Ujerumani kushughulikia suala la ulinzi wa amani, kwamba umoja huo unapitia kipindi kigumu cha kifedha na hilo limeathiri pia operesheni za kulinda amani.
Amesema ni "jambo la muhimu sana" kwa nchi wanachama kutoa michango yao ya kifedha kwa ukamilifu na kwa wakati kukiwezesha chombo hicho cha kimataifa kutimiza wajibu wake.
Rai hiyo ameitoa siku moja baada ya kutahadharisha kuwa Umoja wa Mataifa utalazimika kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kutokana na uhaba wa fedha unaotokana na mageuzi ya kisera ya serikali ya Marekani ambayo tangu kuundwa kwa umoja huo ndiyo imekuwa mfadhili mkubwa.