Guterres akaribisha kuundwa kwa serikali mpya ya Lebanon
10 Februari 2025Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha kuundwa kwa serikali mpya nchini Lebanon, na kuthibitisha kujitolea kwa jumuiya ya kimataifa katika uadilifu wa maeneo, mamlaka na uhuru wa kisiasa wa nchi hiyo.
Msemaji wake Stephane Dujarric, amesema kuwa Umoja wa Mataifa unatarajia kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali mpya ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa usitishaji mapigano.
Dujarric alikuwa akizungumzia makubaliano kati ya Lebanon na Israel yaliyotiwa saini Novemba 27, huku jeshi la Beirut likitarajiwa kutumwa kusini mwa nchi hiyo pamoja na walinda amani wa Umoja wa Mataifa huku Israel ikijiondoa katika maeneo hayo kwa muda wa siku 60.
Waziri Mkuu mpya Nawaf Salam sasa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kusimamia usitishaji mapigano ulio dhaifu wa Israel-Hezbollah na kuijenga upya nchi hiyo.