Guterres ahimiza kuheshimiwa kwa maeneo ya Kongo
16 Februari 2025Amezungumza hayo katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia, siku moja baada ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kuudhibiti mji wa pili nchini humo wa Bukavu.
Guterres amesema mapigano yanayoendelea kusini mwa Kivu yanayotokana na kusonga mbele kwa waasi hao, yanatishia kuisukuma kanda nzima katika vita. Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amehimiza mazungumzo ili kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo.
Vyanzo: Waasi wa M23 wameingia mji wa Bukavu
Kwa upande wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema amezungumza na rais wa Kongo Felix Tshisekedi akisisitiza umuhimu wa Rwanda kutimiza mikakati kadhaa ya haraka ikiwemo kuondoka kwa waasi wa M23 kutoka Bukavu na umuhimu pia wa usitishaji wa mapigano.