Guterres ahimiza kuwepo kwa mshikamano wa kimataifa
19 Februari 2025Guterres amesema hayo jana wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu amani na usalama wa kimataifa .
"Mgogoro wa hali ya hewa unaendelea, ukosefu wa usawa unaongezeka, pamoja na umaskini. Kama linavyofahamu vyema baraza hili, amani inazidi kupotea katika eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu hadi Ukraine, Sudan hadi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kwingineko. Ugaidi na itikadi kali na majanga yanaendelea. Tunaona wingu baya la kutojali sheria likienea."
Soma pia:Guteress awatolea wito viongozi wa G20 kufanikisha mazungumzo ya COP29
Guterres ameongeza kuwa Baraza hilo la Usalama linapaswa kupanuliwa na kuwa na uwakilishi zaidi wa hali halisi ya kijiografia na kisiasa ya leo, pamoja na kuendelea kuboresha mbinu za utendaji za Baraza hilo kulifanya liwe shirikishi zaidi, wazi zaidi, lenye ufanisi, demokrasia na linalowajibika zaidi.