Gulu. Uganda. Waasi waendelea kuuwa raia.
23 Machi 2005Matangazo
Wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada na wananchi wa kawaida wamesema kuwa waasi nchini Uganda wameuwa, kuwakamata watu na wengine kukatwakatwa viungo vyao katika eneo la kaskazini , ambako msimu wa mvua unaleta hali ya hofu mpya kwamba mauaji zaidi yanaweza yakatokea. Miaka 19 ya mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi wa Lord Resistance army LRA, yamesababisha watu zaidi ya milioni 1.6 kuyakimbia maeneo hayo ya kaskazini. Kufuatia kushindwa kwa mazungumzo muhimu mwezi wa desemba , mizozo huu ambao hauonekani kutiliwa maanani duniani unaelekea kuongezeka zaidi.