Greta Thunberg ataka wenzake waachiliwe na Israel
10 Juni 2025Mwanaharakati maarufu wa Sweden, Greta Thunberg, ametowa mwito wa kuachiliwa huru wanaharakati wenzake waliokamatwa na kuzuiliwa, baada ya boti yao ya kupeleka msaada Gaza kuvamiwa na kukamatwa Israel. Mwanaharakati huyo aliyekuwa amezuiliwa na Israel kabla ya kumrudisha kwao, akiwa uwanja wa ndege nchini Ufaransa, akielekea Sweden, amesimulia kilichotokea kwenye safari yao ya kuelekea Gaza:
"Katika eneo la bahari la kimataifa, tulishambuliwa kinyume cha sheria na kutekwa na Israel na kupelekwa kwa nguvu nchini Israel ambako tulizuiliwa na kisha baadhi yetu tukafukuzwa na wengine bado wanazuiliwa. Mambo mengi hatuyafahamu kwa sababu ilikuwa hali ya mkanganyiko na kutoeleweka. Kwa hivyo, hata sijui kinachoendelea. Bado sijakuwa na simu kwa siku kadhaa.''
Thunbergni miongoni mwa wanaharakati 12 waliokuwa wakisafirisha chakula na mahitaji mengine katika Ukanda wa Gaza. Wanaharakati watano raia wa Ufaransa wamewekwa rumande baada ya kukataa kuondoka kwa khiyari nchini Israel.