Polisi Ujerumani yafanya msako mkali dhidi ya kundi la watu
15 Machi 2023Matangazo
Karibu maafisa 400 wa polisi, miongoni mwao polisi ya shirikisho na wa vitengo maalum, walipekua zaidi ya nyumba 20 na ofisi, hasa katika mji mkuu Berlin, lakini pia katika jimbo la mashariki la Saxony-Anhalt.
Shirika la habari la Ujerumani DPA limesema wanaume watano walikamatwa, wanne kati yao mjini Berlin na mmoja katika mji wa Halle, huku washukiwa 12 wakiwekwa chini ya uchunguzi.
Soma pia:Ujerumani kushirikiana na Brazil
Kundi hilo linadaiwa kuwaleta nchini Ujerumani karibu watu 90, wengi wao kutoka Uturuki na Iraq, huku kila mmoja akilipa maelfu kadhaa ya euro. Wengi wa washukiwa hao wana uraia wa Uturuki au Ujerumani, kwa mujibu wa polisi.