Geneva: Mkataba wa plastiki washindwa kufikia makubaliano
15 Agosti 2025Mazungumzo ya kusaka mkataba wakimataifa wa kupambana na takataka za plastiki duniani, yamemalizika hii leo mjini Geneva, Uswisi, bila ya kufikiwa makubaliano.
Baada ya miaka mitatu ya mazungumzo ambapo nchi zipatazo 180 zilikuwa zinakubaliana kwamba takataka za plastiki ni kitisho kikubwa, lakini katika mkutano huo nchi hizo bado zimetofautiana katika masuala kadhaa.
Ingawa mpaka sasa bado haijafahamika jinsi mchakato huo utakavyosonga mbele, lakini mataifa yanayozalisha mafuta yanapinga suala la ukomo wa uzalishaji plastiki zitokanazo na mafuta ya petroli, makaa ya mawe na gesi.
Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo la Ulaya, OECD, limeonya kwamba ikiwa hatua hazitochukuliwa haraka, uzalishaji wa plasitiki utaongezeka mara tatu kufikia mwaka 2060 na kuleta athari kubwa duniani.