Gazeti mojawapo mashuhuri la kaskazini mwa Ujerumani, Ostsee-zeitung...
9 Oktoba 2003 kuhusu kuchaguliwa kwa muigizaji filamu na raia huyu wa asili ya Austria, Arnold Schwarzenegger, kuwa ni Gavana wa California, linasema, halioni sababu ya kufurahia kuchaguliwa kwake, lakini amefanikiwa kuwa Gavana mpya wa California. Baada ya raia huyu wa asili ya Austria kuhamia nchini Marekani kama mgeni wa kawaida, alipata bahati ya kuvumbuliwa na mashirika ya filamu ya kimarekani kuwa ni muigizaji mwenye kipaji. Sababu ya mafanikio yake ni kwa kuwa California inakabiliana wakati huu na haja kubwa ya kuwahakikishia raia wake neema na usalama. Hata ikiwa hii ni kama siasa ya Hollywood, Gavana huyu mpya anatazamiwa kuwaletea mabadiliko wale waliompigia kura mabadiliko.
Nalo gazeti la mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Potsdam, Märkische Allgemeine, linasema: Kuchaguliwa kwa Schwarzenegger ni ishara nzuri ambayo yabidi kutazamwa muhimu wake Baada ya kufanya kazi mbali mbali hapo kitambo na hatimaye kuwa ni mwanabiashara na muigizaji filamu mashuhuri, huu ni ukweli wa mambo, ambao raia wa nchi za ulaya wabidi kuzoea kwanza. Bila kujali yaliyopita, uchaguzi wa Arnorld Schwarzenegger unatoa ishara muhimu ya jinsi alivyojiendeleza kuwa ni mwanasiasa mwenye kipaji cha kuongoza. Anatazamwa ni Gavana-kiongozi ambaye anawapa raia matumaini zaidi kupita watangulizi wake.
Gazeti mashuhuri la Kolon, Kölner Stadt-Anzeiger, kuhusu mada hii linasema: Matokeo ya uchaguzi katika Californioa, yanashuhudia jinsi raia wenye haki ya kupiga kura walivyo na uwezo wa kupitisha maamuzi muhimu, iwapo wanaingiwa na hisia kwamba, yule wanayekwenda kumchagua wana imani kubwa naye ya kuwaletea kile wanachitaka. Ni kutokana na haki ya upigaji kura katika Ujerumani tu kwamba, hapawezi kutokea hali kama hii ya kushangaza iliyotokea katika California.
Gazeti mojawapo mashuhuri la mji wa kusini mwa Ujerumani Munich, Süddeutsche Zeitung, linazingatia mvutano wa mageuzi uliozuka kati ya vyama-ndugu vya upinzani vya CDU na CSU kwa kusema: Waidhinishaji wa mageuzi wa zamani kama Adolf Kolping au wawakilishi wa jumuiya za misaada ya kiutu za kanisa katoliki, hawana nafasi tena zama hizi katika vyama ndugu. Lakini kile kinachokosa hasa ni wafuasi wao walio vijana ambao wangechangia mageuzi yanayotakiwa. Lakini wako wachache ambao wana kipaji kama vile kiongozi wa kundi la chama cha CDU bungeni, Friedirch Merz, wanasiasa mashuhuri wa chama hiki Wolfgang Schhäuble na Wolfgang Bosbach.
Gazeti lingine la kusini mwa Ujerumani, Stuttgarter Zeitung, linazungumzia juu ya chama cha CDU kufika kwenye njia panda, kwa kuandika: Vigogo kama vile Norbert Blüm na Heiner Geissler, wanakaribia kuingia katika maisha ya uzeeni, lakini bado wanaendelea kukisemea chama chao CDU. Baada ya msimamo wa kinyume wa waziri-mkuu wa mkoa wa Bavaria, Edmund Stoiber, huenda ikawa mabwana Blüum na Geissler watakuwa na jukumu muhimu la kukiwakilisha chama chao kwenye mkutano ujao wa kimkoa. Lakini wakati ambao yangeweza kuendelezwa mabishano ya kijadi na chama-tawala cha kansela SPD, umeshapit. Saa ya ukweli wa mambo imeshawadia, ndio maana wenyekiti wa vyama-ndugu vya CDU na CSU, Angela Merkel na Edmund Stoiber, sasa wanawajibika kusimama katika jukwaa moja.
Nalo gazeti lingine la kaskazini mwa Ujerumani, Kieler Nachrichten, kuhusu mada hii linaandika: Kila mara lawama ni zile zile za kawaida, kwanza katika chama-tawala SPD na kishaye vyama vyama-ndugu CDU na CSU. Makundi yanayoelemea upande wa kushoto ya vyama hivi, yanayalaumu makundi yanayoelemea upande wa kulia kwa kushikilia kwamba, hayatilii uzitito kutosha masilahi ya huduma za kijamii. Ni wanasiasa wakongwe pekee kama Geissler, Blüm na Lafontaine, wanaohisi kuthibishwa misimamo yao, lakini wakati wa nadharia zao umeshapita.