Gazeti mashuhuri la mji mkuu Berlin,
12 Januari 2004Matangazo
BERLINER ZEITUNG, kuhusu tangazo la Marekani, kumtazama dikteta wa zamani wa Irak Saddm Hussein, ni mfungwa wa kivita, linaandika: Hii kwa hakika ni habari njema, sio kwa dikteta binafsi pekee, bali tangazo hili linadhirhirisha kwamba, kuhusiana na mzozo wa Itak, Marekani imepiga hatua muhimu, kwenye njia ya kujirejesha katika umoja wa kimataifa. Kwa msaada wa chama cha msalaba mwekundu, Marekani sasa itashikilia sehemu ya kesi dhidi ya Saddam , hadi atakapofikishwa mbele ya mahakhama ya kimataifa. Kwa sababu hii, kuna mambo mawili, yanayodaiwa kutoka upande wa Marekani: Kwanza, inaibidi serikali ya Washington kuchukua hatua bila kuchelewa, ya kuona kwamba, Saddam Hussein atafanyiwa uchunguzi na chama cha msalaba mwekundu cha kimataifa. Na pili, kutekelezwa ahadi, iliyotolewa na waziri wa nje wa marekani, Colin Powel, ya kuwatendea wafungwa wote wa kivita wa Marekani kuambatana na makubaliano ya kimataifa.
Kuhusu uchaguzi wa rais mpya wa Ujerumani, gazeti hili la Berlin, BERLINER ZEITUNG, linasema, mjadala unaoendelea sasa, unaelekea upande usiotakikana linaposisitiza: Vyama vya kisiasa, vinajadili bila kikomo, swala la uchaguzi wa rais mpya wa Ujerumani. Lakini katika swala hili, kuna umbali, ambao vyama vya kisiasa vinaweza kwenda: Wadhifa huu wa rais wa Ujerumani haufanani na wadhifa wa mwanasiasa wa kawaida, na kwa hivyo, mwakilishi huyu wa dola, asitazamwe ni mpatanishi katika ugomvi wa kisiasa. Tunahitaji rais mwenye kipaji, kama alivyokuwa rais wa zamani Richard von Weizäcker.
Tunao watu kadhaa, wanaofaa kuwa wagombea, kwa mfano, mkurugenzi wa shirika la Siemens, Heinrich von Pierer, au hakimu wa zamani wa mahakama ya katiba, Paul Kirchhof.
Nalo gazeti la ESSLINGER ZEITUNG, linazinagia msimamo wa mwenyekiti wa chama kimojawapo cha upinzani, CDU, Angela Merkel, kwa kuandika: Angela Merkel, bado anssitasita. Kwake uchaguzi wa rais mpya, ni ngazi mojawapo kwenye njia kuelekea kugombea wadhifa wa kansela. Kama vyama-ndugu vya CDU na CSU, vitafanikiwa kupatana mgombea wa pamoja, bila ya kutegemea chama-mshirika mdogo cha upinzani cha FDP, basi hapatakuwa na chochote cha kumzuwia, kwenye njia ya kurithi kiti cha Kansela Schröder.
Gazeti la mkoa mdogo wa Saarbrücken, SAARBRÜCKER ZEITUNG, kuhusu hatima ya Bibi Berkel, linandika: Mwenyekiti wa zamani wa chama cha CDU, Wolfgang Schäuble, ndiye aliye na nafasi bora kabisa, ya kuwa mgombea wa vyama-ndugu CDU na CSU. Lakini wakati huo huo, yeye si mtu, ambaye anaweza kutazamwa ni mpatanishi, achilia mbali kashfa zake mfululizo. Bibi Merkel anajua barabara kwamba, kwa sababu hii anategemea sana plani aliyopatana pamoja na mwenyekiti wa FDP,Westerwelle, ati kwa sababu ya uchaguzi katika mkoa wa kaskazini wa Hamburg. Lakini hili si wazo la busara. Ukweli wa mambo ni kwamba, anatafuta mapema msaada wake wa kumteua mgombea anayefaa wa vyama-ndugu. Kwa ufupi, licha ya mabwana Schäble na Töpfer, wakati huu mwenyekiti wa shirila la mazingira la umoja wa mataifa, kuna watu wengine, ambao wanafaa kugombea wadhifa huu wa rais mpya wa Ujerumani.
Gazeti la MINDENER TAGESBLATT, linajishugulisha leo na madai yanayopaazwa na raia wengi wa Ujerumani ya waziri wa afya, Ula Schmidt, kujiuzulu, kuhusiana na mapendekezo yake katika mageuzi ya huduma za afya, kwa kuandika: Ni kweli kwamba, wagonjwa ndio wanaochangia kiwango kikubwa kabisa cha pesa, katika mfumo wa mageuzi haya, lakini inaelekea shabaha yenyewe haitaweza kufikiwa. Ule upunguzaji wa viwango katika mashirika ya bima za afya, haukuweza kutekelezwa, isipokuwa kwa kiwango kidogo tu.
Gazeti mashuhuri la Kolon, KÖLNER EXPRESS, kuhusu mada hii linaandika: Raia wengi wanahamakishwa sana na mageuzi haya ya huduma za afya, iwe ni wakati wa kuonana na daktari, katika kuchangia mashirika ya bima za afya, lakini hasa hasa kwa wagonjwa binafsi. Raia wanahamaki kwa haki, kwa sababu wale walio wanyonge, kwa mfano, wanaopata malipo au mishahara ya chini pamoja na wastaafu, wanashindwa kubeba mzigo huu wa gharama mpya. Kile tunachotaka, yaani hatua kubwa ya maendeleo, kimegeuka katika kesi nyingi, ni sheria ya kigeni, inayosababisha hangaiko kubwa. Kwa sababu hii, kinachofaa hapa, ni kufutiliwa mbali yote yaliyokwishapangwa, na kuanza tena kwa kila kitu kutoka mwanzo.

Matangazo