GAZA: Wanajeshi wajaribu kuyazuia maandamano ya wakaazi wa Gaza
18 Julai 2005Matangazo
Walinda usalama wasiopungua elfu 20 na wanajeshi wamo njiani kuelekea kusini mwa Israel kuzuia maandamano ya wapinzani wanaoupinga mpango wa kuyaondoa makazi ya walowezi wa kiyahudi kutoka mkanda wa Gaza.
Machafuko tayari yamezuka katika eneo hilo huku waandamanaji wakisema watakaidi amri ya polisi na kufanya kila watakaloweza kwenda kwenye makazi ya wayahudi huko Gaza.
Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, ameahidi kufanya kila awezalo kuyakomesha mashambulio ya maroketi na makombora yanayofanywa na wanamgambo wa kipalestina dhidi ya Israel.