Hospitali Gaza yaharibiwa vibaya kwenye shambulio la Israel
13 Aprili 2025Shambulio hilo kwenye Hospitali ya Al-Ahli kaskazini mwa Gaza halikukusababisha vifo lakini limefanyika siku moja baada ya vikosi vya Israel kuchukua udhibiti wa njia muhimu za usalama katika eneo hilo na kuashiria mpango wa kupanua kampeni yake ya kijeshi.
Aidha Qatar, ambayo ilisimamia usitishaji wa mapigano ambao haukufanikiwa, imelaani vikali shambulio hilo ikilitaja kama "uhalifu wa kinyama dhidi ya raia wasio na silaha."
Soma pia: Saudi Arabia yataka Israel ishinikizwe iruhusu misaada Gaza
Wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas imesema leo kwamba takriban Wapalestina 1,574 wameuawa tangu Machi 18, baada ya mpango wa usitishaji mapigano kuposambaratika, na kufanya idadi jumla ya watu waliouawa kufikia 50,944 tangu kuanza kwa vita hivyo.