Aliyekuwa makamu wa rais Kenya Rigathi Gachagua huenda akakamatwa atakaporejea nchini humo, huku viongozi wakimtaka aandikishe taarifa kwa polisi kuhusu madai ya ugaidi aliyoyatoa Marekani. Saumu Njama alizungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Kenya Martin Oloo na kwanza alimuuliza, je, ziara ya Gachagua Marekani ni ziara ya kawaida ya kisiasa au ni mkakati wa kumdhoofisha Rais Ruto?