G20: Ramaphosa ahimiza mshikamano wa kimataifa
20 Februari 2025"Kama kundi la G20 ni muhimu kuzingatia msingi wa sheria za mkataba wa Umoja wa Mataifa, mshikamano wa mataifa na sheria ya kimataifa inapaswa kubakia kuwa kiini cha malengo yetu sote. Inapaswa kuwa kiunganisho kinachotuweka pamoja.''
Kundi la G20 linaloyajumuisha mataifa 19 pamoja na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika, limegawika kwa kiasi kikubwa kuhusu masuala muhimu kuanzia vita vya Urusi nchini Ukraine hadi mabadiliko ya tabia nchi.
Soma pia:Trump amuita Zelensky "Dikteta ambaye hakuchaguliwa"
Rais Ramaphosa amesema mivutano hiyo inatishia mshikamano wa dunia ambao toka hapo uko kwenye hali tete. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amekwepa kuhudhuria mkutano huo kutokana na mvutano kati ya nchi yake na mwenyeji wa mkutano huo, Afrika Kusini, na badala yake atawakilishwa na kaimu balozi wa nchi yake, Afrika Kusini, Dana Brown.